Real wawalaza Barca katika mechi tamu ya El Clasico

Real Madrid imeilaza Barcelona katika mechi ya kusisimua ya El Clasico na kuwapiku mahasimu wao kileleni mwa La Liga. Vinicius Junior alifunga bao katika kipindi cha pili kilichokuwa na nafasi kedekede baada ya kombora la Isco kupanguliwa na kipa wa Barca Marc Andre Ter Stegen na pia mpira wa kichwa kuondolewa kwenye mstari wa lango.

Karim Benzema alipiga iliyopaa juu ya lango na mchezaji nguvu mpya Martin Braithwaite nusra awafungie wageni bao muda mfupi kabla ya Vinicius kuwaamsha mashabiki uwanjani Bernabeu. Mchezaji wa akiba Mariano aliingia katika dakika za lala salama na kuwazika Barca. Real sasa wanaongoza kileleni na mwanya wa pointi moja dhidi ya mahasimu wao.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments