Real yaduwazwa mjini Moscow

100

Mabingwa watetezi Real Madrid waliduwazwa na CSKA Moscow katika mchuano wa Champions League kwa kufungwa bao moja kwa bila. Real sasa wameshindwa kufunga bao katika mechi tatu mfululizo za Champions League huku kuondoka kwa Cristiano Ronaldo kukionekana kuwaathiri miamba hao.

Kwingineko, Jose Mourinho hajashinda mechi nne mfululizo katika uwanja wa nyumbani kwa mara ya nne kabisa katika taaluma yake baada ya Manchester United kutoka sare ya 0-0 na Valencia uwanjani Old Trafford.

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich walifurukuta na kutoka sare ya bao moja kwa moja na miamba wa Uholanzi Ajax.

Manchester City walianzisha kampeni yao kwa kupata ushindi wa dakika za mwisho mwisho dhidi ya Hoffenheim.

Paulo Dybala alifunga hatrick na kuisaidia Juventus kuifunga Young Boys 3-0. Naye Edin Dzeko pia alifunga hatrick katika ushindi wa Roma wa 5-0 dhidi ya Victoria Plzen.

Lyon ilitoka nyuma na kulazimisha sare ya mabao mawili kwa mawili na Shakhtar Donetsk na hivyo kubaki kileleni wa kundi lake pointi moja mbele ya Manchester  City.

AEK Athens ya Ugiriki ilifungwa bao la dakika za mwisho mwisho ya kushindwa kwa mabao 3-2 dhidi ya Benfica.

Tazama maelezo kamili chini ya sehemu ya UEFA kwenye tovuti hii ili kujua msimamo wa makundi

Author: Bruce Amani