Real yatamba dhidi ya Girona

Gareth Bale alifunga bao katika mechi yake ya pili mfululizo na kuisaidia Real Madrid kutoka nyuma na kuilaza Girona 4-1.

Wenyeji hao wa Catalonia walikuwa wamejiweka kifua mbele kupitia bao la Borja Garcia kabla ya Sergio Ramos kusawazisha kupitia penalti baada ya Marco Asensio kuchezewa visivyo katika eneo la hatari.

Real walijiweka kifua mbele kupitia penalti nyingine ambayo bado ilipatikana baada ya Asensio kufanyiwa madhambi lakini mfungaji wakati huu akawa Mfaransa Karim Benzema. Bale baadaye alifunga baada ya kupokea pasi kutoka kwa Isco kabla ya tena kumuandalia pasi safi Benzema ambaye alifunga la nne.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends