Ribery aisaidia Bayern kupunguza pengo dhidi ya vinara Dortmund

47

Franck Ribery alifunga mabao mawili wakati Bayern Munich ilisonga had nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga kwa ushindi wa 3-0 dhidi ya Eintracht Frankfurt.

Kabla ya mapumziko ya msimu wa baridi, Rafinha alifunga bao la tatu katika dakika za mwisho na kuiwezesha Bayern kupunguza hadi pointi sita pengo kati yao na Borussia Dortmund

Awali, RB Leipzig ilirejea katika kinyanganyiro cha ubingwa wa ligi baada ya kuwabwaga Werder Bremen 3-2. Nambari nne Leipzig sasa wako nyuma ya nambari tatu Borussia Moenchengladbach, na pengo la pointi mbili tu.

Schalke, wako katika nafasi ya 13 baada ya kupata ushindi wao wa kwanza katika mechi tano walipowacharaza Stuttgart 3-1.

Fortuna Duesseldorf walipata ushindi wa 1-0 dhidi Hanover 96 ukiwa ndio ushindi wao wa tatu mfululizo na kuwaweka katika nafasi ya 14 kwenye ligi.

Bayer Leverkusen wako nafasi ya tisa baada ya chipukizi mwenye umri wa miaka 19 Kai Hervatz kufunga bao katika ushindi wao wa 3-1 dhidi ya Hertha Berlin. Washika mkia Nuremberg walipigwa 1-0 na Freiburg

Author: Bruce Amani