Ribery ajiunga na Fiorentina baada ya miaka 12 na Bayern

Winga Frank Ribery amesajiliwa rasmi na Fiorentina kama mchezaji huru baada ya kudumu Bayern Munich kwa miaka 12.

Ribery, 36, ameondoka Bundesliga akiwa amefunga magoli 86 katika michezo 273 kwenye miaka hiyo kumi na mbili.

Mfaransa huyo alijiunga na miamba hao wa Ujerumani mwaka 2007 akiwa amecheza jumla ya mechi 425 akishinda mataji 9 ya Bundesliga na Ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2013.

“Nina furaha kubwa kuwa hapa. Naamini tutashinda mataji kwa pamoja,” aliiambia Tovuti rasmi ya Fiorentina.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends