Roben atundika daluga katika klabu ya utotoni Groningen

Arjen Robben ametangaza rasmi kuachana na kabumbu kwa mara ya pili akiwa na umri wa miaka 37.

Winga huyo wa zamani wa Uholanzi mara ya kwanza alitundika daluga mwaka 2019 kabla ya kufutilia mbali maamuzi hayo na kurejea uwanjani kwenye klabu ya Groningen ikiwa ni klabu yake ya kwanza.
Majeruhi na janga la virusi vya Covid-19 vimepelekea hata kandanda lake kutokuwa na nguvu na kuamua kutundika daruga Jana Alhamis Julai 15.
Robben alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu, mawili ya Kombe la Ligi na Kombe la FA akiwa Chelsea.
Lakini pia amecheza PSV Eindhoven, Real Madrid na Bayern Munich, alicheza mechi 96 timu ya taifa akifunga bao 37.
Kupitia ukurasa rasmi wake wa Twitter ameandika kuwa: “Nimeamua kuachana na soka la ushindani, ni maamuzi magumu kuyachukua. Nahitaji kumshukuru kila mmoja kwa mapokezi mazuri”.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares