Robo ya Wajerumani wamtaka Klopp arithi mikoba ya Loew kama kocha wa timu ya taifa

101

Takriban robo ya Wajerumani wanapendelea Jurgen Klopp awe kocha mpya wa timu ya taifa ya Soka ya Ujerumani atakapoondoka kocha wa sasa Joachim Loew ambaye ataachia ngazi baada ya michuano ya kombe la bara la Ulaya mwaka 2020 itakayofanyika msimu wa majira ya Joto.

Uchunguzi mpya wa maoni uliofanywa na YouGov umeonesha asilimia 24 ya Wajerumani 1,618 walioulizwa, walipendekeza Jurgen Kloop ambaye ni kocha wa klabu ya Liverpool ya Uingereza achukue nafasi hiyo, wakati asilimia 9 walimpendekeza aliyekuwa msaidizi wa Loew, Hansi Flick ambaye sasa yuko Bayern Munich.

Majina mengine yaliyopendekezwa ni kocha wa timu ya taifa ya soka ya wachezaji chini ya miaka 21 Stefan Kuntz na Julian Nagelsmann pamoja na Thomas Tuchel wa klabu ya Chelsea ya Uingereza. Jana Klopp alipendekeza Ralf Rangnick akabidhiwe jukumu la kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani, Die Mannschaft.

Author: Bruce Amani