Roger Federer awabwaga Ronaldo, Messi katika kulipwa zaidi duniani

Mwanatenisi anayeshika nafasi ya nne katika orodha ya wachezaji bora wa tennis duniani upande wa wanaume Roger Federer amempiku mwanasoka bora wa dunia Lionel Messi kwa kuwa mwanamichezo anayelipwa zaidi duniani.

Federer ambaye ana uraia wa Uswisi anakuwa mchezaji wa kwanza wa Tenisi kushika nafasi ya kwanza katika malipo ya wanamichezo katika ripoti ya mwaka ambayo hutolewa na Forbes.

Federer, 38, amepanda nafasi nne kutoka alipokuwa anapata £81 awali mpaka hivi sasa anapata zaidi ya £86.

Mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo anapata (£85m) katika nafasi ya pili, Messi nafasi ya tatu (£84m) na Neymar nafasi ya nne (£77.5m), mchezaji wa Mpira wa Kikapu Marekani LeBron James anapata takribani (£71.5m) na anakamilisha tano bora.

Bondia Tyson Fury analipwa zaidi katika nafasi 11 akipata (£46.2m).

Mkimbiza upepo kwa njia ya gari Lewis Hamilton wa Formula One anakamata nafasi ya 13 akipokea £43.7m.

Upande wa wanawake katika mchezo wa Tenisi Naomi Osaka wa Japan ndiye anayeshika nafasi ya kwanza lakini nafasi ya 29 kwa ujumla akimpiku Serena Williams katika listi iliyotolewa na Forbes jana Ijumaa.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends