Roma wasambaratika Old Trafford, Man Utd yatoa kipigo kizito cha 6-2

Manchester United imejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali ya Ligi ya Europa baada ya kushinda bao 6-2 mchezo wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali  mtanange uliopigwa dimba la Old Trafford Leo Alhamis.

Kiungo mshambuliaji Bruno Fernandes na Edinson Cavani wote kwa pamoja wamefunga goli mbili kila mmoja ikiwa Man United wametokea nyuma 2 – 0 na kushinda.

Fernandes aliitanguliza United akimalizia pasi ya mshambuliaji Edinson Cavani kabla ya Roma kupata tuta baada ya Paul Pogba kunawa mpira eneo la hatari kisha Lorenzo Pellegrini akasawazisha bao hilo, dakika chache tena Roma wakatangulia kwa bao la strika mkongwe Edin Dzeko.

Hatimaye mabao mengine yakafungwa na Cavani, Pogba na Mason Greenwood .

Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kuhitaji ushindi au sare ya goli chance kucheza michuano ya Ligi ya Europa hatua ya fainali.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares