Ronaldo ainyemelea rekodi ya kimataifa ya Ali Daei

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na klabu ya Juventus baada ya kufunga goli mbili katika mchezo wa Euro 2020 dhidi ya Hungary kwenye Kundi F ambao Ureno ilishinda 3-0, amevunja na kuweka rekodi mpya ambayo pengine itahitaji muda kufikiwa.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United, Real Madrid na sasa Juventus mbele ya mashabiki 60,000 katika dimba la Puskas Arena alifunga goli moja kwa njia ya penati la pili akikwamisha kwenye utulivu wa hali ya juu.
Goli mbili zikamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga goli 11 katika michuano mitano ambayo ameweza kucheza ya Ulaya, awali rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na staa Michel Platini wa Ufaransa aliyekuwa na bao 9.
Kwa sasa Ronaldo anapaswa kumfikia Ali Daei raia wa Iran mwenye bao 109 katika mechi za kimataifa huku Ronaldo akiwa na bao 106.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares