Ronaldo aipa Juve sare dhidi ya Atalanta, Napoli yazabwa na Inter

Juventus hawawezi kufanya kosa la kumpumzisha Cristiano Ronaldo. Massimiliano Allegri alilazimika kumuingiza uwanjani CR7 katika dakika 25 za mwisho, wakati Juve ilikuwa nyuma 2-1 na pia na wachezaji 10 uwanjani. Nyota huyo Mreno alisawazisha lakini hakuwa na muda wa kutosha kuiokoa kabisa Juve kwa sababu ilitoka sare ya 2-2 na Atalanta siku ya Jumatano.

Ilikuwa mara ya pili pekee msimu huu ambapo Juve imeangusha pointi katika Serie A, lakini sare hiyo imerefusha pengo lake kileleni na pointi tisa mbele ya nambari mbili Napoli ambayo ilishindwa 1-0 na Inter Milan. Beki wa Napoli Kalidou Koulibaly aliiweka timu yake pabaya wakati alipotimuliwa uwanjani na Inter ikafunga bao la ushindi katika dakika ya mwisho na kupunguza pengo kati yake na mpinzani wake. Vijana hao wa Carlo Ancelotti waliumaliza mchezo na wachezaji tisa baada ya Lorenzo Insigne pia kutimuliwa uwanjani.

Wakati huohuo, Lazio ilitinga nafasi ya nne nay a mwisho ya Champions League baa ya ushindi wa 2-0 djidi ya Bologna. Sampdoria iko nafasi ya tano baada ya kuilaza Chievo 2-0, AC Milan ilishuka hadi nafasi ya sita, na kumuwekea shinikizo Zaidi kocha Gennaro Gattuso baada ya kutoka sare tasa na Frosinone

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends