Ronaldo aipa Juventus alama tatu mbele ya Udinese

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo amefunga bao mbili na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Udinese mchezo uliopigwa Leo Jumapili.

Kikosi cha kocha Andrea Pirlo kilijikuta kikiwa nyuma kwa goli la Nahuel Molina mapema kabisa.

Hata hivyo, Ronaldo alipata tuta na kukwamisha mpira nyavuni na kufunga goli la ushindi dakika ya 89 ya mchezo huo.

Matokeo hayo yanaifanya Juve kushika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Serie A na matumaini ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao yamerejea.

Kocha Pirlo anahitaji kufanya kazi vizuri kwani licha ya kushika nafasi ya tatu bado kuna timu ngumu kwenye ratiba yake kwa vile atatakiwa kucheza mechi dhidi ya AC Milan na Inter Milan ili kupata nafasi ya kuingia nne bora.

Inter wamefanikiwa kusitisha utawala wa Juventus kwa kuchukua ubingwa wa 10 mfululizo baada ya leo kuwa mabingwa bila kucheza uwanjani kufuatia Atalanta kutoa sare ya Sassuolo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares