Ronaldo aipa Juventus ushindi wa Supercoppa

Ni mchezaji anayegonga vichwa vya habari kila aendako. Bao la kichwa la Cristiano Ronaldo lilitosha kuwapa Juventus ushindi dhidi ya AC Milan na kunyakuwa kombe le Supercoppa Italiana katika mechi iliyochezwa mjini Jeddah, Saudi Arabia.

Mreno huyo alisukuma kichwa wavuni kutokana na pasi safi ya Miralem Pjanic katika kipindi cha pili bao lililoamua fainali hiyo kati ya vilabu vyenye mafanikio makubwa kabisa katika kandanda la Italia. Lilikuwa bao la 16 la CR7 msimu huu kwa vinara hao wa Serie A.

Patrick Cutrone aligonga besela kwa upande wa Milan. Ni mchezaji huyo aliyesababisha kiungo wa Ivory Coast Frank Kessie kutimuliwa uwanjani.

 

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends