Ronaldo ampa auheni Andrea Pirlo, Juve yabanwa 2-2 na Torino

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo ameisaidia timu yake YA Juventus kuondoka na alama moja kwenye mechi ya dabi dhidi ya Torino Ligi Kuu nchini Italia iliyopigwa Leo Jumamosi Aprili 3.

Kiungo Federico Chiesa alifunga akaunti kwa Juventus dakika ya 13 kabla ya Antonio Sanabria kusawazisha na Sanabria akaongeza lingine kufuatia makosa ya walinzi.

Mpira wa kichwa wa Ronaldo kunako dakika ya 79 ambalo awali lilikataliwa na mwamuzi wa pembeni kabla ya maamuzi ya video saidizi kwa waamuzi kuruhusu bao hilo kuwa halali.

Juventus sare hiyo inawafanya wawe alama tisa nyuma ya vinara Inter Milan ambao wanacheza na Bologna Seria A leo.

Wakati Torino wako nafasi ya 17 alama mbili eneo salama.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares