Ronaldo amtetea Solskjaer United

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo anaamini kuwa timu hiyo inahitaji muda zaidi wa kutulia baada ya kupoteza mwelekeo kwenye msimu huu.

United kwa sasa wako nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England alama tano pungufu ya kinara Chelsea wakiwa wamekusanya alama moja pekee kwenye mechi tatu.

Wakati wakiwa nje ya mchezo, Manchester United inayonolewa na kocha Ole Gunnar Solskjaer itawakaribisha Liverpool Jumapili ya Octoba 24 huku wapinzani wao wakishika nafasi ya pili na alama 18.

“Tuko kwenye wakati ambao kwa maoni yangu Manchester United imefanya mabadiliko kadhaa ya wachezaji, wameninunua mimi(Ronaldo), Varane na Sancho”, alisema Ronaldo mwenye umri wa miaka 36.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo amejiunga kwa mara nyingine na United akitokea Juventus, wakati Raphael Varane amesajiliwa kutoka Real Madrid na winga Jodan Sancho kutokea Borrusia Dortmund.

“Tutakuwa tunabadilika siku hadi siku, itafika siku hata uchezaji wetu pia utabadilika”.

Kauli ya mchezaji huyo imezua mjadala hasa kutokana na presha kubwa kwa kocha Ole Gunnar Solskjaer.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends