Ronaldo aondoka Old Trafford na ushindi

52

Manchester United walizidiwa maarifa wakati Juventus yake Cristiano Ronaldo ilipowashinda vijana hao wa Jose Mourinho katika mchezo wa klabu bingwa Ulaya uliopigwa uwanjani Old Trafford.

Ilikuwa ni miaka 15 na nusu tangu mara ya mwisho timu hizi mbili Manchester United na Juventus kukutana, ingawa kwenye mchezo wa Jumanne kila mmoja aliyetazama anafahamu sasa ni nani kati ya miamba hao wawili yuko katika afya njema.

Manchester iliikaribisha Juventus katika mchezo ambao ulishuhudia pasi ya Ronaldo ikizalisha goli la kuongoza lilofungwa na Paulo Dybala katika ushindi wa goli 1-0 huku yakiwa matokeo mazuri tofauti na ilivyotabiriwa.

Kwingineko

Lyon ilishindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Hoffenheim baada ya kuongoza kwa dakika 90 kabla ya mshambuliaji wa Hoffenheim, Joelton kufunga goli katika dakika za lala salama katika mchezo uliochezwa Ujerumani.

Andrej Kramaric aliifungia Hoffenheim goli mbili kipindi cha kwanza dakika chache baada ya Bertrand Traore kufunga goli la kuongoza kwa upande wa Lyon.

Lyon kutoka Ufaransa ilifanikiwa kuongoza katika kipindi cha pili baada ya goli la Tanguy NDombele (57) na Memphis Depay (67) ingawa baadae yakafutwa kwa goli la dakika za majeruhi alilolifunga Joelinton ambalo lilikuwa na kusawazisha.

Bayern Munich ilifunga magoli 2 katika dakika tatu za kipindi cha pili nchini Ugiriki dhidi ya AEK Athens na hivyo kushinda 2-0.

Mabingwa hao wa Ujerumani walifunga kwa faulo maridhawa kutoka kwa Javi Martinez katika ya dakika ya 61, ambapo Robert Lewandowski alifunga goli la pili lililoifanya Bayern kuwa nafasi ya pili sawa na Ajax kwa tofauti ya goli za kufunga na kufungwa.

Hii ni baada ya Ajax nayo kushinda goli 1-0 dhidi ya Benfica.

Real Madrid imefanikiwa kuendelea kuongoza kundi G baada ya kushinda 2-1 dhidi ya Viktoria Plzen katika uwanja wa Bernabeu kupitia Karim Benzema, na Marcelo.

AS Roma inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo kwa tofauti ya goli za kufunga na kufungwa, ambapo jana pia Roma iliibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya CSKA Moscrow kupitia magoli mawili ya kipindi cha kwanza yake Edin Dzeko na lile la Cengiz Under dakika ya 50.

Author: Bruce Amani