Ronaldo Ataka Kuuzwa Man United

218

Staa wa Ureno Cristiano Ronaldo ameomba kuondoka Manchester United endapo klabu hiyo itapokea ofa nzuri kwenye kipindi hiki cha dirisha kubwa la usajili.

Maombi ya Ronaldo yanajiri licha ya kocha wa sasa wa timu hiyo Erik ten Hag kuthibitisha awali kuwa mchezaji huyo bado yupo kwenye mipango yake kwa msimu ujao.

Ronaldo 37, alirejea Old Trafford msimu uliopita 2020/21 akitokea Juventus ambapo sasa amekuwa akitamani kuondoka huku ikielezwa kuwa mashetani wekundu kutokuwa kwenye nafasi ya kushiriki Uefa ni moja ya sababu.

United ilimaliza nafasi ya sita kwenye msimamo wa EPL ambapo watacheza Europa Ligi na bado staa huyo wa zamani wa Real Madrid ana mkataba wa mwaka mmoja.

Author: Bruce Amani