Ronaldo atavalia jezi namba 7 Man United

Cristiano Ronaldo atavalia jezi namba saba katika kikosi cha Manchester United, namba ambayo ilikuwa inavaliwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Edinson Cavani ambaye sasa atavaa jezi namba 21 iliyokuwa inavaliwa na Daniel James.

Ronaldo, 36, kabla ya kujiunga na Manchester United awamu ya pili aliwai kuvaa jezi namba hiyo ambapo alifanya makubwa na kuwa mmoja ya wachezaji ambao waling’aa kipindi cha babu Sir Alex Ferguson.

Ronaldo ataanza kufanya mazoezi na Man United baada ya siku tano za kujitenga mwenyewe, Alhamis hii alitolewa kwenye majukumu ya timu ya taifa kutokana na kupigwa “stop”.

“Sikutegemea kama ingekuwa rahisi kupata tena namba saba, namshukuru sana Cavani kwa kukubali kuniachia namba, ni ishara kubwa kwangu”.

Ronaldo alikamilisha uhamisho wa kushitua kutua Old Trafford katika siku za mwisho za dirisha kubwa la usajili ambapo anaweza kuwa sehemu ya mchezo wa Manchester United dhidi ya Newcastle United Septemba 11.

Ronaldo alifunga goli mbili kwenye ushindi wa goli 2-1, na kuweka rekodi yake mpya akiipiku rekodi ya Ali Daei mwenye goli 109 wakati Ronaldo akiwa na 111 ngazi ya taifa.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares