Ronaldo atupia hat-trick ya haraka zaidi, Juve ikishinda Cagliari 3-1

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo amefunga goli zote tatu za Juventus katika ushindi wa 3-1 wa mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A dhidi ya Cagliari na kuandikisha rekodi ya kufunga goli tatu yaani hat-trick ya mapema zaidi.

Ronaldo, 36, alifungua akaunti ya magoli kwa kichwa kabla ya shuti la mguu wa kulia na hatimaye penati ambayo ilihitimisha furaha kwa upande wake hasa baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Porto.

Giovanni Simeone aliipatia timu yake goli la kufutia machozi.

Juventus wanakaa nafasi ya tatu, wanaizidi timu ya Atalanta alama tatu ambao ni wanne.

Inakuwa hat-trick yake ya haraka Serie A lakini akiwa nchini Hispania na Real Madrid mwaka 2015 aliweka rekodi kama hiyo ingawa ilichukua muda mfupi zaidi.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares