Ronaldo atupia mbili, Juventus ikiichapa kibonde Crotone 3-0

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo amefunga magoli mawili ya kichwa akiisaidia timu yake ya Juventus kushinda bao 3-0 dhidi ya Crotone katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Italia na kuendeleza hofu kwa timu zilizo juu yake.

Ushindi huo unaifanya Juventus kuwa alama nane nyuma ya vinara Inter Milan ambao walijiimarisha kileleni baada ya kuitandika AC Milan bao 3-0 wikiendi iliyopita.

Ronaldo alianza kufunga goli kupitia mpira wa beki wa kushoto wa timu hiyo Alex Sandro kabla ya kufunga bao lingine akitumia vyema mpira wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Aaron Ramsey, likiwa bao lake la 70 katika Serie A ndani ya miaka miwili na nusu.

Crotone inakuwa klabu ya 78 kati ya zile zilizopokea goli la Ronaldo.

Weston McKennie alifunga goli la tatu kwa Juve.

Ronaldo anafikisha goli 18 na kumpiku mshambuliaji wa Inter Milan Romelu Lukaku ambaye nae yuko kwenye ubora mkubwa.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares