Ronaldo atupia tatu, Ureno ikiichapa Luxembourg 5-0

Timu ya taifa ya Ureno imetoa kipigo kizito kwa taifa la Luxembourg cha goli 5-0 kwenye mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 mtanange uliopigwa dimba la Estadio Algarve huku staa Cristiano Ronaldo akifunga bao tatu (hat-trick).

Ushindi ambao unaifanya Ureno kupanda mpaka nafasi ya pili, nyuma ya vinara Serbia ambao watakutana kwenye mechi ya mwisho katika Kundi A.

Ronaldo, 36, alifunga goli mbili za haraka kwa njia ya penati kabla ya kufunga bao la tatu jioni kabisa na kufanya kuwa mchezaji mwenye goli nyingi dhidi ya timu moja (9), mabao 115 ya kimataifa, hat-trick hiyo inakuwa ya 58 katika taaluma yake mpaka sasa.

Mabao mengine yakafungwa na Bruno Fernandes na Joao Palhinha.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends