Ronaldo sasa rasmi Manchester United

Cristiano Ronaldo amekamilisha uhamisho wake kutoka Juventus na kujiunga na Manchester United ikiwa ni kurejea tena Old Trafford baada ya miaka takribani 10.

United wamekubali kulipa kiasi cha pauni milioni 12.85 sawa na Euro milioni 15 ambapo inaweza kuongezeka kwa Euro milioni 8.
Ronaldo ameingia kandarasi ya miaka miwili ambapo mkataba huo unakipengele cha kuongeza mwaka mmoja wa kuendelea kukitumikia kikosi cha Mashetani Wekundu.
“Manchester United ni klabu ya kipekee iliyo na nafasi yangu moyoni mwangu” alisema staa huyo.
“Nimepata faraja kubwa kwa namna ambavyo nimekuwa nikipokea jumbe za pongezi tangia dili langu kukamilika siku ya Ijumaa”.
Ronaldo, ambaye alifunga bao 118 katika mechi 292 kwenye kipindi cha kwanza cha kuitumikia Manchester United kabla ya kuondoka mwaka 2009, “Nina shauku kubwa kurudi Old Trafford na kukutana tena na mashabiki”.
Kocha Ole Gunnar Solskjaer akizungumzia ujio wa Ronaldo amesema anakosa hata maneno mazuri ya kumuelezea, ubora wa mchezaji huyo, “Sio tu mchezaji mkubwa pia na utu”.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares