Ronaldo: Perez hakunihitaji tena Real Madrid

Cristiano Ronaldo amesema aliamua kuhama Real Madrid msimu huu kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Uhispania Florentino Perez, alimuona tu kama mbinu ya kutengeneza pesa.

“Aliniona tu kama katika uhusiano wa kibiashara. Nanjua hilo. Alichoniambia kamwe hakikutoka moyoni,” mshambuliaji huyo Mreno ameliambia jarida la Kandanda la Ujerumani.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 alijiunga na Juventus ya Italia kutoka Real mwezi Julai kwa kitita cha euro milioni 100 na ameisaidia klabu yake mpya kuwa na mwanzo mzuri ambapo hawajashindwa mpaka sasa katika Serie A msimu huu. Amewafungia mabingwa hao wa Italia mabao saba katika mechi 10

“katika miaka ya kwanza minne au mitano, (nikiwa Real) nilikuwa na hisia za kuwa ‘Cristiano Ronaldo’. Baadaye hisia zikapungua. Rais aliniona katika macho ambayo hayakutaka kusema kitu hicho hicho, kana kwamba sikuwa muhimu kwao,” alisema.

Hatua ya Real kutoijaza nafasi yake katika soko la uhamisho imegonga mwamba na mabingwa hao wa Ulaya sasa wako katika nafasi ya tisa katika La Liga huku kocha mpya Julen Lopetegui akitarajiwa kutimuliwa.

Kocha wa zamani Zinedine Zidane alikuwa ameionya klabu hiyo kuwa mabadiliko makubwa yalihitajika, na akaondoka Real katika kile ambacho kinaonekana kuwa ni uamuzi wa busara.

Mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ureno anaridhika na uamuzi wake wa kuondoka ikizingatiwa namna mambo yanavyokwenda uwanjani Santiago Bernabeu msimu huu.

“Kama ingekuwa ni hela, ningehamia China, ambako niketia kibindoni mara tano Zaidi. “Sikuja Juve kwa ajili ya pesa. Nilipata kiasi sawa na hicho Real Madrid,n ahata labda Zaidi, lakini tofauti ni kuwa katika Juve, walinihitaji. Waliniambia hilo na wakaliweka wazi.”

Author: Bruce Amani