Rooney atupa karata ya ubingwa wa Euro kwa Ufaransa

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Timu ya Taifa ya England Wayne Rooney amesema anaamini England itafanya makubwa katika mashindano ya Euro 2020 ingawa ameipa ubingwa timu ya Ufaransa akisema “iko kitimu zaidi”.

Rooney ameyasema hayo katika makala yake kwenye gazeti la Times akisema England ina kikosi kizuri chini ya kocha Gareth Southgate lakini vipaji vikubwa vya vijana vimekosa uzoefu tofauti na Ufaransa ambayo ina muunganiko mzuri tena wa muda mrefu kutokea kwenye fainali ya Kombe la Dunia la Urusi mwaka 2018.

Amesema mbali na uzoefu, pia kikosi cha kocha Didier Deschamps kina wachezaji wengi ambao wako kwenye ubora wao, ambapo amewataja wanandinga kama N’golo Kante, Paul Pogba, Kylian Mbappe, Antoine Griezmann, Raphael Varane, Karim Benzema na Hugo Lloris.

Mbali na kutaja kikosi cha Ufaransa na ubora wake, Rooney hakusita kumtaja N’golo Kante kama sehemu muhimu kwa kocha Deschamps akisema ni mchezaji mwenye ufanisi.

Amesema Kante ni zaidi hata ya Yaya Toure wa Barcelona na Manchester City hata Claude Makelele pia kutokana na mwendelezo mzuri wa kiwango.

Timu ya Taifa ya Ufaransa iko kundi moja pamoja na Ujerumani ambayo watafungua imba Juni 15, Ureno, na Hungary.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares