Ruben Dias ajifunga Man City mpaka 2027

34

Beki wa kati wa Ureno Ruben Dias ameongeza mkataba mpya wa kuendelea kukitumikia kikosi cha Manchester City ambapo sasa mkataba wake utamalizika mwishoni mwa msimu wa 2027.

Beki huyo tangia kujiunga na Man City amekuwa na wastani mzuri wa kiwango ambapo msimu uliopita alitwaa tuzo binafsi ikiwa ni ishara ya ubora wake kwenye eneo la ulinzi la Man City.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, alijiunga Manchester City akitokea Benfica mwaka 2020 mwezi Septemba kwa kandarasi ya miaka sita kwa dau la pauni milioni 65.

Aliisaidia kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, kushinda taji la Ligi Kuu England na Kombe la Carabao, alitajwa pia kama mchezaji bora wa mwaka kupitia tuzo za Chama cha Waandishi wa Habari.

Author: Asifiwe Mbembela