Rugby – Kenya yatinga michezo ya Olimpiki

62

Timu ya taifa ya Kenya ya mchezo wa raga ya wachezaji kila upande, Shujaa imefuzu katika michezo ya Olimpiki mwaka ujao jijini Tokyo nchini Japan, baada ya kuilaza Uganda alama 31- 0 jioni hii katika uwanja wa Bosman jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Mbali na kufuzu katika michezo hiyo, Kenya pia ni mabingwa wa Afrika. Mataifa 14 yalishiriki katika mashindano haya. Miongoni mwa mataifa hayo ni pamoja na Zimbabwe, Madagascar, Zambia, Tunisia, Senegal miongoni mwa mengine.

Author: Bruce Amani