Ruvu Shooting Yavuna Pointi Moja Mbele ya Azam

29

Ruvu Shooting wamevuna alama moja dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mtanange uliopigwa dimba la Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani kwa kulazimisha sare ya goli 1-1.

Elias Maguri alianza kuifungia Ruvu Shooting dakika ya 82, kabla ya Rodgers Kola kuisawazishia Azam Fc dakika ya 90.

Azam FC inafikisha pointi 37, ingawa inabaki nafasi ya nne ikizidiwa tu wastani wa mabao na Namungo FC inayoshika nafasi ya tatu, wakati Ruvu sasa ina pointi 28 nafasi ya 12 baada ya wote kucheza mechi 26.

Mechi iliyotangulia leo, bao pekee la Vincent Abubakar dakika ya 46 limeipa Coastal Union ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mbeya City leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Coastal inafikisha pointi 34 na kusogea nafasi ya nne, wakati Mbeya City inabaki na pointi zake 32 nafasi ya nane baada ya wote kucheza mechi 26

Author: Asifiwe Mbembela