Safari ya mastaa hawa 7 Afcon 2019 imekatikia njiani

Kabla ya mashindano ya Afcon 2019 kuanza kulikuwa na majina yaliyotamba sana kwenye ngazi ya klabu, mafanikio yao ilitegemewa kutokea katika Timu za taifa lakini sasa mambo yameenda kombo kwa uwezo wao kushindwa kuonekana.

Hapa Amani sports news inakuletea majina ya mastaa 7 walioshindwa kuzisaidia timu zao:-

  1. Eric Choupo-Moting, Staa wa Cameroon na PSG.

Kabla ya Afcon kuanza aliisaidia klabu yake kutwaa ubingwa wa Ligue 1 licha ya kutopata nafasi ya kutosha. Choup-Moting kama nahodha wa Cameroon alishuhudia timu yake ikiondolewa na Nigeria hatua ya 16 bora kwa kufungwa goli 3-2.

  1. Naby Keita, Staa wa Guinea na Liverpool.

Alikuwa sehemu ya kikosi cha Liverpool iliyoshika nafasi ya pili EPL, akaisaidia timu hiyo kufika fainali ya Uefa licha ya kupata majeraha hatua ya nusu fainali. Aliporudi kuitumikia Guinea ameshindwa kuhamishia mafanikio yale kwenye timu ya taifa licha ya kutokuwa “fit” 100%.

  1. Arthur Masuaku, Staa wa Congo na West Ham.

Ni beki wa kutumaini ndani ya Wagonga Nyundo wa London, West Ham United lakini alipoingia Congo amefanikiwa kucheza mchezaji mmoja tu kisha akaishia bechi baada ya kiwango hafifu dhidi ya Uganda, ikishuhudia timu hiyo ikiondolewa hatua ya 16 bora na Madagascar kwa matuta.

  1. Sadio Berahino, Staa wa Burundi.

Uzoefu wa kucheza EPL katika klabu ya Stoke City ilitegemewa na Warundi kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri. Berahino alipofika Misri ameshindwa hata kufunga goli moja katika michezo 3.

  1. Mbwana Ally Samatta, Staa wa Tanzania na Genk

Alitwaa kiatu cha dhahabu Genk kwa kufunga goli 23 pamoja na tuzo ya mchezaji bora ndani ya ligi ya Ubeligiji kwa wachezaji wanatokea Afrika. Alibeba matumaini ya Watanzania lakini mambo yameshindwa kwenda sawa. Akaishia kufunga goli 1 tu.

  1. Hakim Ziyech, Staa wa Morocco na Ajax

Alikuwa sehemu ya kizazi bora cha Ajax msimu 2018/2019 baada ya kuishia hatua ya nusu fainali ya Uefa kwa kutolewa na Tottenham. Mafanikio aliyoyapata Ajax yameshindwa kutokea Morocco huku akikosa penati mechi ya 16 bora dhidi ya Benin dakika za lala salama.

  1. Mohammed Salah, Staa wa Misri na Liverpool.

Ikiwa fainali zinafanyika nyumbani, Wamisri waliamini MO Salah ataweza kubakiza taji nyumbani na kuwa taji lao la nane lakini mambo yamemwendea kombo. Salah akiwa na Liverpool alikuwa kinara wa magoli EPL,(22) akiifikisha fainali Liverpool na kushika nafasi ya pili.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments