Salah Aipa Ushindi Liverpool kwa Nottingham Forest

53

Mohamed Salah ameipa Liverpool ushindi kwa kufunga bao dakika za mwishoni lililoisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Nottingham Forest mchezo uliopigwa dimba la Anfield Jumamosi.

Ushindi huo muhimu kwa Liverpool umeisaidia kufufua matumaini ya kushiriki mashindano ya Uefa msimu ujao ambapo sasa wanashika nafasi ya saba wakiwa na alama 50.

Mabao ya Liverpool yamefungwa na Diogo Jota aliyeingia kambani mara mbili pamoja na hilo la Salah ambaye ameweka chuma dakika za jioni.

Wakati yale ya Nottingham Forest iliyopo nafasi ya 19 na alama 27 yamefungwa na Neco Williams na Morgan Gibbs-White.

Matokeo hayo ni hatari kwa Nottingham Forest kwani wapo nafasi ya kushuka daraja.

Author: Bruce Amani