Babu wa Western Stima kocha bora wa Agosti, Septemba KPL

Kocha wa kilabu ya  ligi ya Premier ya Kenya, Western Stima FC Salim Babu  ametajwa kuwa kocha bora wa miezi  ya Agosti na Septemba  na kampuni ya  Bima ya Fidelity.

Babu amewapiku makocha wenzake katika ligi Zedekiah Otieno wa KCB na Steven Pollack wa   Gor Mahia  ambao walipata alama sita na saba mtawalia . Babu  ambaye ndiye maneja wa kwanza kushinda tuzo hiyo msimu huu amejinyakulia  kombe lake maalum na Runinga.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends