Salzburg yainyeshea mvua ya mabao Genk ya Samatta

98
Mbwana Samatta amefanikiwa kuwa mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa barani Ulaya baada ya kuanza kwenye kikosi cha KRC Genk ya Ubeligiji dhidi ya Red Bull Salzburg ya Austria.
Samatta licha ya kuwa sehemu ya kikosi cha Genk lakini pia ameingia kwenye orodha ya wafungaji bora wa michuano hiyo baada ya kufunga goli moja katika kipigo ilichokipata klabu ya Genk cha goli 6-2 ukiwa mchezo wa kwanza hatua ya makundi.
Kwa maana hiyo, nahodha huyo wa kikosi cha Taifa Stars amekuwa mtanzania wa kwanza na kuungana na Victor Wanyama wa Kenya na Oliech ukanda wa Afrika Mashariki kucheza michuano hiyo mikubwa ngazi ya klabu.
Mbali na rekodi ya Mbwana Ally Samatta katika mashindano hayo, klabu ya Genk imeanza vibaya baada ya kukung’utwa goli 6-2.

Author: Bruce Amani