Samatta aendelea kuitikisa Europa League

67

Sio ajabu kwamba jina lake linahusishwa na vilabu kadhaa vya Premier League ya England. Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta maarufu kama Samagoal anaendelea kubusu katika michuano ya Europa League, baada ya kuifungia klabu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji mabao mawili katika ushindi wao wa 4-2 dhidi ya Besiktas ya Uturuki.

Samatta alifunga bao la kwanza dakika ya 23 na kisha akaongeza la pili dakika ya 70 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Joakim Maehle mara zote mbili.

Besiktas walikomboa bao moja dakika ya 74 kupitia Vagner Loveawazisha dakika ya 74, lakini Genk wakaongeza mabao mengine mawili kupitia Dieumerci Ndongala (81′) na Jakub Piotrowski (83). Vagner Love aliifungia Besiktas bao jingine dakika ya 86 na mechi ikamalizika 4-2.

Sasa, nyota huyo wa Tanzania amefunga mabao matatu katika hatua ya makundi Europa League, ingawa alikuwa amefunga mengine matano mechi za muondoano za kufuzu za kabla ya hatua ya makundi.

Alifunga bao moja dhidi ya Malmo FF 20 Septemba. Katika mechi za kufuzu Europa League msimu huu, alifunga mabao mawili dhidi ya Lech Poznan, bao moja kila mechi.

Mnamo 23 Agosti 2018 Samatta, alifunga ‘hat-trick’ dhidi ya Brøndby IF katika Europa League kwenye mechi ambayo walishinda 5-2, na baadaye mechi ya marudiano akawafunga bao moja. Samagoal sasa amefikisha manane jumla ya mabao aliofunga mpaka sasa katika Europa League msimu huu

Ni kutokana na hali yake nzuri ambapo sasa anahusishwa na taarifa za kutafutwa na klabu za West Ham United, Everton na Burnley nchini England

Author: Bruce Amani