Sancho akutwa na majeruhi mazoezi arudishwa Man United

Winga wa Manchester United na England Jadon Sancho ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambacho kilikuwa kinaendelea na maandalizi ya mchezo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Andorra na Poland kwa sababu ya majeruhi madogo (amegongwa eneo).

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, aliumia kwenye mazoezi ya wiki hii ambapo pia alikosa mechi ya Alhamis ambayo England walishinda mbele ya Hungary.
Baada ya majeruhi hayo, jopo la madaktari limemruhusu kwenda klabuni kwake kwa ajili ya matazamio zaidi huku kocha Gareth Southgate akibakiwa na jeshi la watu 23.
Hata hivyo, kwa maelezo ya awali inaonekana Sancho atakuwa sehemu ya kikosi cha Manchester United kitakachocheza mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Newcastle United Jumamosi ya Septemba 11.
England itacheza dhidi ya Andorra Jumapili Septemba 5 kabla ya kumalizia na Poland Jumatano.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares