Sancho apiga ‘hat-trick’, Dortmund yaichapa Paderborn, Munich yainyeshea Fortuna Dusseldorf

Winga Jadon Sancho ameandikisha rekodi ya aina yake baada ya kufunga goli tatu kwenye mechi moja na kuwa hat trick ya kwanza katika maisha yake, lakini anakuwa mchezaji wa kwanza kutokea Uingereza kufunga goli tatu tangu miaka 31 iliyopita alipofunga Brian Stein.

Goli hizo tatu amezifunga katika mchezo ulioishuhudia Borrusia Dortmund ikiiadhibu Paderborn goli 6-1. Alikuwa ni Thorgan Hazard aliyefungua karamu ya magoli ungwe ya pili, kisha Sancho akafunga goli la kwanza tangu Februari 29, Achraf Hakimi na Marcel Schmelzer waliingia katika ubao wa wafungaji kisha Sancho akaongeza goli mbili zilizohitimisha ushindi mnono wa Dortmund ambao uliwa wa kujifariji baada ya kupokea kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Bayern Munich wiki moja iliyopita.

Goli pekee la Paderborn lilifungwa na Uwe Hunemeier kwa njia ya penati. Hata hivyo ushindi huo haukuwa na maana yoyote zaidi ya kufurahia wao wenyewe kwani siku moja kabla Bayern Munich walitoka kutoa kichapo kikali cha goli 5-0 dhidi ya Fortuna Dusseldorf.

Ubora wa Roberto Lewandowski waendelea kutikisa bara la Ulaya, apiga mbili kwenye ushindi huo. Pengo la pointi saba limeendelea baina ya miamba hiyo miwili katika soka la Bundesliga.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends