Sancho aweka historia na kuisaidia Dortmund kurejea kileleni

Mshambuliaji wa England Jadon Sancho ameweka historia kwa kufunga mabao mawili wakati Borussia Dortmund ikiichapa Mainz 2 – 1 na kupanda kileleni mwa Bndesliga angalau kwa siku moja

Sancho mwenye umri wa miaka19 ndiye mchezaji mwenye umri mdogo sana kuwahi kufunga mabao 11 katika Bundesliga.

Robin Quaison aliipa Mainz bao na kuwarejesha mchezoni lakini Dortmund wana kila sababu ya kumshukuru kipa wao Roman Burki aliyefanya kazi ya ziada katika dakika za mwisho mwisho na kuwapa BVB pointi zote tatu.

Dortmund sasa wamekamata usukani na pengo la pointi mbili mbele ya mabingwa Bayern Munich, ambao wanaweza kurejea kileleni kama watashinda Jumapili ugenini dhidi ya Fortuna Dusseldorf Jumapili

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends