Sancho hatolimwa adhabu kwa kuonyesha mshikamano maandamano ya Floyd

Winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho na wachezaji wengine wa Bundesliga hawataadhibiwa kutokana na kuonyesha wazi kutokubaliana na ubaguzi rangi dhidi ya mauaji ya Mmarekani George Floyd.

Mchezaji huyo raia wa England alitoa jezi yake iliyokuwa na ujumbe wa ‘Haki kwa George Floyd’ baada ya kufunga goli tatu dhidi ya Paderborn.

Floyd, aliuawa katika mji wa Minneapolis Mei 25 baada ya kubanwa shingo kwa kutumia goti na askari mmoja ambaye baadae alifutwa kazi.

Mchezaji mwenza wa Dortmund kutokea Morocco Achraf Hakimi pia alivaliwa jezi ya ndani wenye ujumbe sawa na ule ulioandikwa na Sancho, Marcus Thuram wa Borrusia Monchengladbach alipiga magoti baada ya kufunga goli kama ishara ya kumkumbuka Floyd.

Ripoti ya Chama cha Soka Ujerumani (DFB), inasema hakuna hatua zozote za kinidhamu ambazo zitachukuliwa dhidi ya wachezaji hao wanne.

Katika kanuni na sheria za FIFA zinawataka wachezaji kutoonyesha ujumbe wowote wenye maneno ya kisiasa, lakini kutokana na hilo hatuna uwezo wa kuwa adhabu amesema Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu duniani Gianni infantino.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends