Sare ya Atalanta na Sassuolo, yawapa ubingwa Inter

Inter Milan wamefanikiwa kuvunja udhibiti wa Juventus wa taji la Ligi Kuu nchini Italia kwa kushinda taji hilo baada ya Atalanta ambao wanashika nafasi ya pili kutoa sare dhidi ya Sassuolo.

Inter wanabeba ubingwa huo baada ya takribani miaka 11 bila ubingwa huku Juventus ambao walikuwa mabingwa watetezi wakitawala anga hizo.

Miamba hiyo ya soka la Milan wako kileleni kwa tofauti ya alama 13 baada ya kuvuna pointi tatu dhidi ya Crotone Jana Jumamosi.

Inter walimaliza wa pili msimu uliopita kwa tofauti ya alama moja, kocha Antonio Conte amehitimisha rasmi utawala wa miaka tisa mfululizo.

Ubingwa huo ni wa kwanza kwa Inter tamgia Jose Mourinho afanye hivyo mwaka 2010.

Unakuwa ubingwa wa nne kwa Conte baada ya awali kushinda mara tatu mfululizo na Juventus mwaka 2011-2014, pia alishinda taji la EPL Chelsea 2017.

Author: Asifiwe Mbembela

Sharing is caring!

0Shares