Sare ya West Bromwich dhidi ya Wolves yatia doa matumaini ya vijana hao wa Sam Allardyce kusalia EPL

Sare ya goli 1-1 ambayo West Brom wameipata kwa Wolverhampton Wanderes imeifanya timu hiyo kuwa mguu ndani mguu nje kwenye Ligi ya EPL.

Sifa ambazo kocha Sam Allardyce amekuwa akizipata zimeshindwa kufanya kazi kwa awamu hii kutokana na ugumu wa michezo msimu HUU. Ili kubakia EPL kocha Allardyce anahitaji ushindi mechi nne zote zilizosalia akianzia safari hiyo kwa Arsenal Jumapili.

Magoli ya leo kwa timu zote mbili yamefungwa na Fabio Silva ungwe ya kwanza kabla ya Mbaye Diagne kusawazisha na kuwapa alama moja ambayo ni muhimu zaidi kwao.

Kocha Nuno Espirito Santo alikuwa kwenye nafasi ya kukiongoza kikosi chake cha Wolves kushinda lakini haikuwa hivyo kutokana na ubora wa mlinda mlango Sam Johnstone ambaye alisevu mpira wa Adama Traore na Nelson Semedo.

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares