Sarri aweka rekodi mpya Chelsea

130

Maurizio Sarri amekuwa Kocha wa kwanza wa Chelsea kutoshindwa katika mechi 10 za Ligi kuu ya England mfululizo baada ya The Blues kuikandamiza Burnley 4-0.

Magoli ya Chelsea yamefungwa na Alvaro Morata, Ross Barkley, Willian na Ruben Loftus-Cheek na kuifanya Chelsea kupaa mpaka nafasi ya pili, nyuma ya Liverpool kwa alama 2 na ushindi huo umepelekea Sarri kuweka rekodi hiyo.

Hakuna Kocha yeyote wa The Blues ambaye amewai kufundisha  mechi 10 za ligi kuu bila kupoteza, hii ni mara ya kwanza kwa kocha wa huyo ambaye pia amewai kuwa Meneja wa zamani wa Napoli kufanya hilo.

Chelsea imeshinda michezo saba kati ya 10 ya mwanzo dhidi ya Huddersfield, Arsenal, Newcastle, Bournemouth, Cardiff, na Southampton na pia iligawana alama kwenye michezo mitatu dhidi ya West Ham, Liverpool na Manchester United.

Kipindi chote hicho Chelsea imesalia bila kupoteza hata kwenye kombe la Eroupa katika michezo mitatu ya mwanzo uwezo huo pia waliuendeleza baada ya kuifunga Liverpool kwenye ya Carabao Cup kwenye hatua za mwanzo.

Author: Bruce Amani