Sasa ni rasmi, Serie A kuanza kutimua vumbi tena Juni 20

Waziri wa michezo wa Italia Vincenzo Spadafora ameruhusu shughuli za michezo kuendelea kufanyika tena kuanzia Juni 20.

Serie A ilisitishwa Marchi 9 ambapo wakati ligi ikisitishwa mabingwa watetezi Juventus ilikuwa inaongoza ligi kwa tofauti ya alama moja huku raundi 12 zimesalia kutamatisha kandanda nchini humo.

Wachezaji walianza mazoezi mwanzoni mwa mwezi Mei ambapo katikati ya mwezi huu wakaanza mazoezi katika makundi madogo madogo.

Mei 20, Shirikisho la Soka Italia (FIGC) ilipanga tarehe ya mwisho ya Agosti 20 kama mwisho mwa kucheza mashindano ya ndani ya msimu wa 2019/20.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends