Semenya awekewa kizingiti kingine na IAAF

Shirikisho la Kimataifa la Riadha, IAAF limepinga uamuzi wa mahakama ya Uswisi, kumruhusu mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya, kushiriki katika mashindano wakati rufaa yake ikiendelea dhidi amri ya kumtaka apunguze kiwango chake cha homoni za kiume.

Baada ya pingamizi ambalo IAAF imethibitisha kulipokea, jaji ataamua ikiwa Semenya ambaye ameshinda mara mbili medali ya dhahabu katika mbio za mita 800, anaweza kuendelea kukimbia mbio za mita 400 hadi maili moja bila kupatiwa dawa za kupunguza homini ya testesteron.

Mwezi Mei, Semenya alipata ushindi wa muda katika mzozo wake na Korti ya Usuluhishi Michezoni, CAS, baada ya mahakama ya Uswisi kuiahirisha kwa muda amri ya IAAF dhidi yake. IAAF inasema inataka kulinda michezo ya tabaka la wanawake kwa misingi ya kimaumbile, na sio ya utambulisho wa kijinsia.

Author: Bruce Amani

Facebook Comments