Senegal na Tunisia zinaongoza katika ubora wa mchezo wa soka barani Afrika baada ya Shirikisho la soka duniani FIFA, kutangaza viwango vya ubora wa nchi mbalimbali mwezi huu.
Licha ya kuongoza Afrika, Tunisia imeshuka nafasi tatu huku Senegal nayo ikipanda nafasi 24 duniani.
Misri imeshuka, nafasi 20 na sasa ni ya 65 duniani, baada ya matokeo mabaya katika michuano ya kombe la dunia mwezi Julai nchini Urusi. Barani Afrika, Misri inashikilia nafasi ya 11.