Serie A kuwapima wachezaji mwezi Mei tayari kwa kuanza kampeni ya Ligi

Shirikisho la Mpira wa Miguu Italia lina matumaini wachezaji wataanza kupimwa kubaini kama watakuwa na maambukizi ya Corona au la mwanzoni mwa mwezi wa tano tayari kwa kuendelea na msimu.

Ligi kuu nchini Italia Serie A imesema tangu Marchi 9 kutokana na janga la kidunia.

Hakuna tarehe maalumu iliyopangwa ya kuendelea kwa michuano hiyo lakini michezo raundi 12 na ratiba ya mechi hazijachezwa mpaka sasa kumalizika kwa msimu wa mwaka huu.

“Punde hali ya ugonjwa itakapotengamaa, ligi itaendelea na tutamaliza msimu pia”, we alisema Rais wa Shirikisho Gabriele Gravina.

“Tutaanza, ninaimani kuwa mwishoni mwa mwezi wa tano tunaweza kuanza kuwajaribu wachezaji ili zoezi la kuingia kambini kwa wachezaji lianze.

Tutacheza hata kiangazi hatuna siku ya mwisho ya kumalizika kwa ligi, tunachoangalia ni msimu kumalizika kwa namna yoyote ile”, aliongeza Gabriel Gravina Rais wa Shirikisho.

Tarehe ya mwisho ya mwezi wa tatu bado Juventus walikuwa vinara wa Seria A wakati Lazio ikiwa nafasi ya pili kwa tofauti ya alama moja, tofauti ya alama tisa na Inter Milan iliyonafasi ya tatu.

Wiki iliyopita, Ujerumani ilikuwa nchi ya kwanza kwa bara ya Ulaya wachezaji wake kurejea mazoezi chini ya uangalizi maalumu kuhakikisha maambukizi hayaendelei kwa wachezaji hao.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends