Serie A wakusudia kumaliza msimu Agosti 20 kabla ya msimu mpya kuanza Septemba mosi

Shirikisho la Mpira wa Miguu Italia (FIGC) limepanga tarehe ya mwisho ya kumalizika kwa msimu huu kuwa Agosti 20. Septemba Mosi msimu mpya utaanza rasmi.

Msimu huu ulisitishwa katikati ya mwezi Marchi kutokana na janga la virusi vya Corona. Hata hivyo FIGC wanaamini wataweza kukamilisha mechi zilizosalia katika madaraja matatu tofauti.

Mechi 12 zimesalia kutamatisha msimu wa SERIE A, ambapo Juventus wanaongoza mbio za ubingwa huku vibibi vya Turin vikichuchumilia taji la tisa mfululizo

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends