Sevilla yapoteza nafasi ya kushikilia usukani

Sevilla ilishindwa kuendelea kudhibiti usukani wa La Liga Jumapili baada ya kutoka sare ya 1-1 na Alaves, na hivyo kuwaruhusu Barcelona kupanda tena kileleni mwa msimamo wa ligi.

Winga wa Alaves Jony alifyatua kombora hadi wavuni na kuwaweka kifua mbele katika dakika ya 37, licha ya mamaliko kutoka kwa Sevilla kuwa Jonathan Calleri alikuwa katika nafasi ya kuotea wakati alipotoa pasi iliyosababisha bao hilo.

Wissam Ben Yedder aliisawazishia Sevilla katika dakika ya 78. Sare hiyo na maana kuwa Alaves, ambao waliwazaba mabingwa wa Ulaya Real Madrid 1-0 mapema msimu huu, na Atletico Madrid ndizo timu pekee ambazo hazijashindwa mechi katika uwanja wa nyumbani msimu huu.

Sevilla sasa wako nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi na pointi 27 baada ya mechi 14, moja nyuma ya vinara Barca. Atletico Madrid ni wa tatu na pointi 25, wakati Alaves ni wan ne na 24 pointi moja juu ya nambari tano Real Madrid.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends