Shabana FC yatinga ligi ya kitaifa Kenya NSL

127

Klabu ya Shabana imerejea katika Ligi Pana ya Kitaifa nchini Kenya  kwa maana ya National Super League, NSL. Shabana ambayo inajivunia halaiki ya mashabiki baada ya timu za AFC leopards na Gor Mahia, imerejea katika ligi hiyo ya NSL baada ya kuifunga Mwatate magoli 7-6 kupitia kwa matuta ya penaliti.

Mechi hiyo iliamuliwa kwa njia ya penaliti baada ya sare ya kufungana goli 1-1 katika muda wa kawaida. Nahodha wa Shabana Wycliffe Nyanoech amewahakikishia mashabiki kuwa watarejea katika ligi ya KPL mwaka 2020. “Tumerudi na lengo letu ni kucheza ligi ya KPL mwaka 2020!” amesema nahodha huyo

Author: Bruce Amani