Sheikh Khaled afikia makubaliano kuinunua Newcastle

Bilionea Sheikh Khaled Bin Zayed All Nehayan mwenye makao yake Dubai ameweka wazi kufikia makubaliano ya kuinunua klabu ya Newcastle United inayoshiriki ligi Kuu nchini England.

Sheikh Khaled ni tajiri mwenye vinasaba na tajiri wa klabu ya Manchester City Sheikh Mansour.

Klabu hiyo hivi sasa iko chini ya mmiliki Mike Ashley ambaye amekuwa katika klabu hiyo tangu mwaka 2007, miaka 12 akishuhudia timu ikishuka mara mbili kucheza ligi daraja la kwanza. Ashley ana hisa asilimia 41 katika klabu hiyo

Kupitia taarifa rasmi ya klabu hiyo na kundi la matajiri hao kutoka Dubai imeandikwa makubaliano yetu na Ashley yamefikia hatua nzuri ya kuinunua Newcastle United yenye makao yake St. James.

‘Tunaweza kuthibitisha kuwa wawakilishi katika nafasi za juu kabisa za uongozi katika Kampuni yetu ya Sheikh Khaled Bin Zayed Al Nahyan wanafanya mazungumzo na mmiliki wa Newscastle  Mike Ashley na timu yake juu ya kuinunua timu hiyo”.

“Tunaweza kusemea tumefikia hatua nzuri ya kwenda kuandika historia katika klabu yenye utamaduni wa mda mrefu na kuijenga kuwa shindani zaidi”.

Bilionea Sheikh Khaled bin Zayed Al Nehayan (Binamu wa mmiliki wa Manchester City, Sheikh Mansour), yuko katika kilele katika utajiri wake kwani msimu uliopita alijaribu kuinunua Liverpool ingawa dili hilo liligonga mwamba akiwa anatarajia kuwekeza kiasi cha £2 bilioni.

Endapo Newcastle United itafanikiwa kununuliwa na tajiri huyo inaweza kuingia kwenye zile timu 6 za juu kwenye msimamo wa EPL katika kushindana kwenye soko la usajili kama ilivyo kwa Manchester City, Liverpool, Chelsea.

Ugumu sasa waweza kuongezeka zaidi kutokana na nguvu ya fedha inayoweza kwenda kutumika katika mambo mbalimbali ama nyenzo kama hizo.

Author: Bruce Amani