Shikalo rasmi kuikabili Zesco United

Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limethibitisha kuwa mchezaji wa Yanga Mkenya Farouk Shikalo anaweza akaanza kuitumikia klabu hiyo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kuwasili kwa vielelezo vya kazi ndani ya Yanga.

Shikalo alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao walishuhudia dakika 180 za mechi zao dhidi ya Township Rollers jukwaani baada ya leseni yake kuchelewa kutoka.

Wachezaji wengine ambao walikosa leseni ni pamoja na straika Mcongo David Molinga na Mustapha Suleiman ambaye ni raia wa Burundi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten amesema “Muda wowote kutoka sasa leseni ya Shikalo itawasili baada ya Caf kuruhusu atumike kwenye mechi inayokuja, lakini kwa Mustapha na Molinga wao bado na hatuwezi kuwatumia hadi tutakapofika makundi,” alisema Ten.

Yanga itacheza na Zesco United Septemba 14 mwaka huu Dsm mtanange wa Ligi ya mabingwa Afrika kuwania kufuzu makundi ya michuano hiyo.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends