Shujaa kuanza mazoezi ya michuano ya IRB

Timu ya taifa ya Kenya ya raga ya wachezaji saba kila upande sasa itaanza mazoezi ya michuano ya kimataifa ya IRB Sevens wiki ijayo, siku kadhaa baada ya kufuzu katika michecho ya Olimpiki ya 2020. Shujaa iliilaza Uganda 31-0 katika fainali za Africa 7s mwishoni mwa wiki mjini Jo Berg, Afrika Kusini na kunyakua tikiti hio.

Shujaa wanarejea kwa mara ya pili baada ya kuwakilisha Kenya katika michezo ya Rio 2016. Timu hio imerejea nyumbani leo na watapambana na Afrika kusini, Uingereza na Uhispania katika kundi D la michezo ya IRB.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends