“Sijui kama PSG ni sehemu nzuri ya kucheza” Mbappe

Mkataba wa winga wa Kifaransa na Paris St-Germain Kylian Mbappe unamalizika mwishoni mwa msimu ujao 2021/22 lakini mchezaji huyo amesema hajui kama klabu hiyo ni sehemu sahihi ya kucheza.
Winga huyo anayetajwa kama mrithi wa mikoba ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika kutesa anga la Ulaya akiwa na miaka 22 amekuwa akihusishwa mara kadhaa kujiunga na Real Madrid.
Akizungumza akiwa kwenye majukumu ya timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya Euro 2020, Mbappe ameweka wazi kuwa anafuraha ndani ya PSG ingawa hana uhakika wa kubakia klabuni hapo.
“Natakiwa kufanya maamuzi sahihi ambayo siku zote ni magumu kwangu, natakiwa kuwa makini kabla ya kuamua”.
“Niko sehemu ambayo napapenda, ninapojisikia vizuri, lakini ni sehemu sahihi kwangu? Kwa kweli sijui”, alisema mchezaji huyo wa zamani wa Monaco.
Naweza kuondoka lakini natakiwa niondoke bila kuwa msaliti kwa viongozi na mashabiki wa PSG

Author: Bruce Amani

Sharing is caring!

0Shares